Isaiah 11:12-13

12 aAtainua bendera kwa mataifa
na kuwakusanya Waisraeli walioko uhamishoni;
atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika
kutoka pembe nne za dunia.
13 bWivu wa Efraimu utatoweka,
na adui wa Yuda watakatiliwa mbali;
Efraimu hatamwonea Yuda wivu,
wala Yuda hatakuwa na uadui na Efraimu.
Copyright information for SwhNEN